Na. Kadama Malunde
Chama cha waandishi wa habari za vijiji RUJAT wiki hii kinatarajia kufanya kongamano la kitaifa la waandishi wa habari vijijini
Kwa mujibu wa viongozi wa chama hicho kongamano hilo litafanyika jijini Dodoma Oktoba 31 likifuatiwa na mkutano mkuu wa wanachama.
Mwenyekiti wa RUJAT Neville Meena na Katibu Bw. Prosper Kwigize wameeleza kuwa kongamano hilo litakuwa na jukumu la kuwakutanisha waandishi wa habari za vijiji kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara kujadili hali ya upashanaji habari nchini Tanzania.
Aidha kuhusu mkutano mkuu imeelezwa kuwa pamoja na mambo mengine wanachama watapokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya chama hicho pamoja na kufanya uchaguzi wa viongozi.
katibu wa RUJAT Ndugu Kwigize amebainisha kuwa Chama hicho chenye dhima ya kuhakikisha jamii vijijini inafikiwa na huduma za habari na mawasiliano, kimekuwa na desturi ya kualila wadau kwa ajili ya kujadili masuala ya kisekta.
Kongamano kama hilo lilifanyika mwaka 2023 ambapo wadau walishiriki mijadala mbalimbali iliyowasilishwa na Bank ya Biashara TCB, NMB, NHIF na TANAPA
FUNGUA HAPA KUTAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA






