Waumini wa Kiislamu wahimizwa kuchangamkia fursa za kiuchumi

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Waumin wa kiislam nchini wametakiwa kutambua fursa za kiuchumi zilizipo nchini na kuanzisha miradi ya ujasiliamali na kiuchumi ili kufaidika na fursa hizo badala ya kuisha bila shughuli maalum na kuwa omba omba.

Imam wa Masjidi Maamur Upanga jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa baraza la Ulamaa Taifa la Baraza kuu la Waisalm Tanzania (BAKWATA), Shekhe Issa ametoa kauli hiyo mkoani Kigoma katika Hauli yaa miaka 70 ya kumbukumbu ya kifo cha Mwanazuoni na Mwalim wa dini mkoani Kigoma, Mohamed Ibrahim Kabeke iliyofanyika Msikiti wa kabondo Ujiji mjini Kigoma.

Shekhe Othman alisema kuwa hata vitabu vya dini ikiwemo Quran inahimiza waumini kutawanyika kwenye uso wa dunia kwa ajili ya kutafuta riziki kukidhi mahitaji yao ya kila siku hivyo amewataka waumin wa dini ya kiislam nchini kujifunza masuala ya elimu ya fedha na biashara na kuanzisha shughuli za kiuchumi na ujasiliamali.

Imam wa Masjidi Maamur Upanga jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa baraza la Ulamaa Taifa la Baraza kuu la Waisalm Tanzania (BAKWATA), Shekhe Issa Othman akizungumza katika Hauli hiyo

Akizungumza kufanyika kwa maadhimisho hayo kwa niaba ya Familia ya Shekhe Ibrahim kabeke, Shekhe wa mkoa Mwanza, Hassan Kabeke alisema kuwa maadhimisho hayo (Hauli) imefanyika miaka yote tangu kifo cha Mwanzuoni huyo mwaka 1956 na kwamba maadhimisho hayo yamefanyika kuenzi mchango wake mkubwa katika mafundisho ya dini ambayo yametoa wahadhiri, walimu wa dini na Mashekhe mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Kiongozi wa timu ya Madaktari waliokuwa wakisimamia zoezi la upimaji afya, Shaban Magorwa alisema kuwa waumini wa kiislam Zaidi ya 200 wamejitokeza kupima afya huku uniti 61 za damu zikikusanywa kutoka kwa waumini wa kiislam waliohudhuria Hauli ya kumbukumbu ya miaka 70 ya kifo cha Mwanazuoni na Mwalim Mkubwa wa dini mkoani Kigoma Marehemu Shekhe Mohamed Ibrahim Kabeka iliyofanyika Ujiji mjini Kigoma.

Also Read  MO awapa somo la maisha wanachuo RUCU, kutumia fursa za kiuchumi

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *