Become a Member

by

PAKUA FOMU YA MAOMBI YA UANACHAMA CHINI

Ukurasa huu ni kwa ajili ya waandishi wa habari na wahariri wanaopenda kujiunga na Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini (The Rural Journalists Association of Tanzania – RUJAT) imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya hiyari chini ya Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi.
Baadhi ya wanachama wa RUJAT katika Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kongamano la mwaka 2026
MALENGO YA RUJAT NI PAMOJA NA
1. Kuwa na mtandao imara wa wanataaluma wanaowasiliana nankusaidia kutaaluma na kijamii
2. Kuwezeshana na kujengeana uwezo kitaaluma
3. Kuratibu na kuwezesha waandishi wa habari kupata fursa mbalimbali za ruzuku za kazi au utafiti vijijini na kusaidia wanachama kupata ufadhili  wa masomo ndani na nje ya nchi
4. Kuchunguza, kuandika na kutangaza habari ambazo zinagusa maslahi ya umma hususani ambazo huwa hazipewi kipaumbele na vyombo vingi vya kitaifa na kimataifa
5. Kuwa tovuti na kurasa za za mitandao ya kijamii ambazo zitatumika kuchapisha habari zote za vijijini zitakazoandikwa vizuri kwa kuzingatia taaluma na kukusaidia kufikia wasomaji ndani na nje ya nchi na kukuwezesha kufahamika
6. Kusimamia maadili na kudhibiti upotoshaji wa habari
7. Kusogeza huduma za habari vijijini na kuchochea uwajibikaji kwa umma na kusisimua maendeleo.
Endapo unapenda kuwa mwanachama wa RUJAT unatakiwa kujaza fomu na kutekeleza maelekezo yaliyopo ndani ya fomu hiyo
Kupata fomu bofya kwa maandishi hapo chini