Mufti wa Tanzania atahadharisha kuhusu matumizi ya AI katika mafundisho ya dini

Na. Fadhil Abdallah, Kigoma

Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi ameonya waumini wa kiislam nchini kuwa maakini na matumizi ya teknolojia ya akili Mnemba (AI) katika kufuatilia mafundisho ya dini kwenye mitandao ya kijamii kwani mafundisho mengine yanapotosha na kwenda kinyume na mafundisho ya dini na Hadithi za Mtume Muhamad (SAW).

Shekhe Mkuu alisema hayo akizindua msikiti mkubwa wa Ijumaa Masjidi Nuru katika Mji wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo alisema kuwa dunia imepiga hatua kubwa katika matumizi ya Akili Mnemba kwenye mambo mbalimbali na kwamba zipo chanel na mitandao ambaayo imekuwa ikitoa mafundisho yenye maana na kujenga jamii.

Mufti Zuberi alisema kuwa zipo pia chanel na mitandao ambayo inapotosha mafundishio ya dini na hadhithi za mtume hivyo kuwaonya waumini wa kiislam kuwa makini wanapoingia kwenye mitandao ya kijamii kujua chanzo cha watu wanaoweka maudhui hayo kwenye mitandao hiyo na namna wanavyoaminika kwa mafundisho wanayotoa.

Msikiti mpya wa Ijumaa Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma

Akifungua msikiti mkubwa wa ijumaa katika mji mdogo wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Mufti Xuberi amewataka viongozi wa dini kutumia misiki na madrasa kufundisha maadili na tabia njema kwa waumini wao na kwamba masikiti isiwe kwa ajili ya kusali pekee bali iwe msingi wa kujenga maadili mema ya jamii

Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzania Dk.Abubakar Zubeir akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa ujenzi wa msikiti wa ijumaa Nguruka (Masjidi Nuru) wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Seif Hamisi wakati Mufti alipouzindua msikiti huo Septemba 18.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mfadhili wa ujenzi wa Msikiti huo, Kailima Ramadhani ambaye ni Mkurugenzi wa Tume Huru ya uchaguzi Tanzania (INEC) alisemaa kuwa amejtolea kusaidia ujenzi wa msikiti huo kutokana na hali aliyoona misikiti ya eneo hilo ambapo aliweza dhamira ya mamabo matatu ikiwemo ujenzi wa Msikiti na madras ya kufundisha dini na masomo mbalimbali ya kiislam.

Also Read  TanzanEye yafadhili kituo cha tiba ya macho, wagonjwa milioni 2 kutibiwa kila mwaka Kigoma

Msikiti huo wenye uwezo wa kuchukua waumini 300 kwa wakati mmoja utakuwa na vyumba viwili vya madrasa kwa ajili ya kufundisha dini, eneo la kutawadhia sambaamba na ujenzi wa vyoo matundu 10, chumbaa cha kuoshea maiti,ofisi ya Imam wa Msikiti, vyumba viwili vya Maktaba,kisima chenye urefu wa mita 150 , matanki mawili ya kuhifadhia maji na vituo sita vya kugawa maji kwa wananchi wa eneo hilo ambayo yatatolewa bure huku kukiwa na taa 12 za Mwanga wa jua zilizojengwa kuzunguka eneo la msikiti.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *