Na. Anna Robi, RUJAT Mtwara
SERIKALI kupitia Bodi ya Korosho Nchini (CBT) inatarajia kubagua asilimia 30 ya korosho zote zitakazozalishwa kwa msimu wa 2026/2027.
Mkurungezi wa Masoko na Udhibiti Ubora CBT Revelian Ngaiza amesema msimu huu uzalishaji unatarajiwa tani 750,000.
“Kwa msimu 2026/2027 lengo la kubagua korosho nchini ni asilimia 30 ya uzalishaji,” amesema.
Ngaiza amesema mkakati huo umelenga kukuza soko la ndani ya korosho, kwa.kuongeza thamani kwenye zao la korosho.
Amesema bodi imejipanga kuhamasisha ubaguaji na ulaji wa korosho nchini kwa kutumia njia mbalimbalj ikiwemo kuandaa matamasha ya kitaifa ,kongamano na marathon kutoa elimu umuhimu wa ubaguaji na ulaji wa korosho nchini.
Amesema Tanzania kwa sasa ina viwanda vikubwa , kati na vidogo 26 vya kubagua korosho vyenye uwezo wa kubagua korosho asilimia 20 ya korosho ghafi zinazozalishwa nchini.
“Mwaka huu tuna viwanda vikubwa viwili vinamalizika kujengwa mwaka huu na hivi vikikamilika vitasaidia kuongeza uzalishaji wa korosho zilizobaguliwa,” amesema.
Mwaka 2010, serikali kupitia Wizara ya Kilimo naCBT ilianzisha upya mikakati ya kuhamasisha wawekezaji na vikundi vidogo kujenga viwanda. Kwa sasa, serikali inatekeleza mkakati wa kuhakikisha asilimia 100 ya korosho zinabanguliwa nchini ifikapo msimu wa 2029/2030, ikihusisha ujenzi wa kongani kubwa ya viwanda vya kubangua korosho mkoani Mtwara.






