Utoaji wa lesini za Biashara Mafinga una dosari- TAKUKURU

Na. Hafidhi Ally, RUJAT Iringa

Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Mufindi wamewasilisha ripoti ya matokeo ya ufuatiliaji wa mfumo wa utoaji leseni za biashara katika Halmashauri ya Mji Mafinga, ikibainisha changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ili kuboresha huduma hiyo kwa wananchi.

Akiwasilisha ripoti hiyo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU, Daudi Tweve, amesema baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao bila leseni wamekuwa wakitumia ukosefu wa elimu kuhusu taratibu za upatikanaji wa leseni kama sababu, hivyo ameshauri kuwekwa kwa utaratibu utakaosaidia kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri hiyo, Luis Ndumbaro, amependekeza kuundwa kwa kikosi kazi cha wataalamu kutoka Idara za Biashara, Sheria, TEHAMA na Mipango kitakachokuwa na uwezo wa kutoa majibu na ufafanuzi wa hoja mbalimbali zinazohusu leseni wakati wa kufanya operesheni za ufuatiliaji kwa wafanyabiashara.

Naye Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Mji Mafinga, CPA Fatuma Ridhiwani, ameishukuru TAKUKURU kwa kufanya ufuatiliaji huo na kubaini mapungufu ambayo yameisaidia menejimenti kupata picha halisi ya changamoto zilizopo katika mfumo wa utoaji leseni na kuweka mikakati ya kuzitatua.

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Peter Ngussa, ameelekeza kuandaliwa kwa timu itakayowashirikisha wafanyabiashara na watendaji wa kata ili kubaini wafanyabiashara wanaodaiwa leseni.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuandaliwa kwa vipeperushi vyenye majibu ya maswali yanayohusu leseni za biashara pamoja na kuwekwa kwa utaratibu wa kutoa matangazo ya elimu kwa wananchi kila robo mwaka.

Hatua hizo zinatarajiwa kuongeza uelewa wa wafanyabiashara kuhusu taratibu za upatikanaji wa leseni na kuboresha usimamizi wa mfumo wa utoaji leseni katika Halmashauri ya Mji

Also Read  Kheri James atoa maagizo mazito Mufindi-ataka uwajibikaji

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *