Amani ni matokeo ya Haki, Katiba mpya ni misingi ya haki na amani, Dkt. Nchimbi

Na. Gerwin kwigize -Dar-es-salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuhakikisha Katiba mpya inapatikana, ndio maana suala hilo limewekwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuahidi kulitekeleza.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa 15 wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) uliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam mapema jana.

Dkt. Nchimbi Amesema suala la Tanzania kuwa na Katiba mpya limejadiliwa tangu mwaka 1992 mara baada ya kuanza kwa vyama vingi, lakini Serikali ya Awamu ya Sita imeahidi kulitekeleza kwa manufaa ya wananchi.

Amewasihi wananchi kuibeba ajenda hiyo kwa uzito mkubwa ili iweze kutekelezwa katika kipindi hiki na kwamba inatakiwa uchanguzi mkuu wa 2030 na wa serikali za mitaa 2029 ufanyike chini ya Katiba Mpya.

Aidha, Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuzingatia suala la haki, kwani ndio msingi wa amani katika Taifa lolote lile.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na wajibu wa kuhakikisha wananchi wanaishi kwa usalama bila hofu.

Onesmo Ole Ngurumwa, Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC)

Awali, Mratibu wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania Wakili Onesmo Ole Ngurumwa akitoa maelezo kuhusu utendaji wa THRDC mbele ya Makamu wa Rais na wanachama wa mtandao wa watetezi kutoka zaidi ya asasi 100 kutoka pande zote za nchi, alisisitiza kuwa Tanzania inahitaji mageuzi katika sheria zake

Ngurumwa alibainisha kuwa suala la Tanzania kukamilisha mchakato wa kuwa na katiba mpya hali paswi kupuuzwa kwakuwa yapo mambo ambayo nchi inapaswa kuyapa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinazingatiwa na kwamba katiba mpya ni mwarobaini

Also Read  Dkt. Mwigulu akoleza maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki -Morogoro

Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) umefanya mkutabno wa 15 tangu kuasisiwa kwake ukiongoza zaidi ya mashirika ya kiraia 300 ambayo pamoja na mambo mengine yanafanya kazi za kutekeleza afua mbalimbali za maendeleo na utetezi wa haki.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *