Halmashauri ya Kasulu Mji ina pesa ya kutosha kuinua wajasiriamali

Na. Mwandishi wetu, Kasulu

Katika juhudi za mh. *Dr Samia* kulitizama anga la makundi ya vijana wanawake na walemavu hajaishia tu kutizama Leo tena kafanya jambo halmashauri ya mji kasulu

Kupitia juhudi za zinazofanywa na ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI na *MH.SHEMDOE* na wizara ya vijana chini ya kijana *MH. Nanauka* pamoja na ofisi ya maendeleo ya jamii na makatibu watendaji Nia yenu kasulu kuinuka inazidi kutimia katika kuhakikisha vijana walemavu wanapata maendeleo

Akiongea kwa kina na ushawishi mkubwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji kasulu *MWL VUMILIA SIMBEYE* juu ya ufuatiliaji wa mikopo ya 10% amesema pesa hizo zitatumika kama ambavyo selikali ya awamu hii inazielekeza na zaidi ya mil.200 kupangwa kutolewa kwa vikundi vyote vilivyokidhi vigezo na pia sambaba na utaratibu wa namna ya kupata mkopo huo

Aidha kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya mji kasulu ilitumia zaidi ya mil.600 kwa kutoa mikopo hiyo.

Amesisitiza kua elimu juu ya mikopo hiyo itazidi kutolewa kwa wanufaika hivyo watu na wadau wasiogope kuja kuchukua. Akishiriana na mratibu wa mikopo hiyo *ndg GODFREY JEREMIAH* na wadau mbalimbali amesema tayari mifano wazi kwa makundi yaliyonufaika kama bwawa la samaki kata ya msambala ufugaji wa kuku na makundi mengi tu katika miradi mbalimbali

Aidha kwa upande wa wananchi Bado juhudi za kumuunga mkono na shukrani wanazoweza kufanya ni kuzidi kutoa kodi kwa moyo na kusema Asante sana *DR SAMIA* kwa kuleta mfereji huu wa maendeleo. Na usimamizi uliotukuka kutoka kwa mkurugenzi *mwl VUMILIA SIMBEYE*

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *