- AHIMIZA ONGEZEKO LA TIJA KWA UZALISHAJI MAZAO KWA KUTUMIA MBEGU BORA
Na. Mwandishi wetu, Morogoro
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba amewataka wadau wa sekta ya Kilimo Nchini kuhakikisha wanaongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya shambani kwa kutumia mbegu bora.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati alipotembelea maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Maarufu kama Nanenane yanayofanyika kanda ya Mashariki Hapa Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kutembelea baadhi ya mabanda na kujionea shughuli mbalimbali za wakulima,wafugaji na hata wafanyabiashara ,bila kusahau baadhi ya Halmashauri hapa Nchini zilizojitokeza kuonesha bidhaa zao kwenye maonesho haya.







