Rais wa Zanzibar afunga mafunzo maalumu ya makada wa Chama Cha Mapinduzi- ahimiza Uzalendo

Na. Mwandishi wetu, Zanzibar

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema mafunzo ya makada wakufunzi ni muhimu katika kuimarisha Chama kuanzia ngazi za chini, kwa kuhakikisha misingi, itikadi, historia na maadili ya CCM vinaeleweka na kufikishwa kwa wanachama kwa usahihi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 30 Septemba 2026, wakati akifunga Mafunzo ya Wakufunzi wa Makada wa CCM Awamu ya Pili yaliyofanyika Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema jumla ya makada 840 wamepatiwa mafunzo kupitia programu hiyo, huku akiwataka wakufunzi hao kuimarisha elimu ya Chama, matumizi ya teknolojia ya kidijitali, pamoja na kuimarisha mashina na matawi katika kusikiliza na kushughulikia kero za wanachama na wananchi.

Awali, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, akiwasilisha taarifa kuhusu mafunzo ya kuongeza uelewa wa itikadi ya CCM, Ujenzi wa Chama na Kuongeza wanachama wapya, yaliyohitimishwa leo Septemba 30, 2026, katika chuo cha Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Tunguu, mjini Zanzibar.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, akiwasilisha taarifa kuhusu mafunzo ya kuongeza uelewa wa itikadi ya CCM

Mafunzo hayo ya awamu ya pili yamehitimishwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Katika hotuba yake, Kihongosi amesema usaili wa makada waliohudhuria mafunzo hayo ulizingatia uelewa wa historia, muundo, misingi na itikadi ya Chama, uwezo wa kujenga na kuwasilisha hoja, mbinu za ufundishaji, maadili na nidhamu pamoja na uwezo wa kuendeleza elimu ya Chama.

Amesisitiza kuwa mfumo huo uliwezesha kuweka viwango vinavyofanana vya uteuzi kabla ya hatua ya mafunzo.

Also Read  CultivAid yatoa mafunzo kwa wakulima mkoani Dodoma
Makada wahitimu wa mafunzo ya ukufunzi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka mkoa wa Kigoma waliohitimu na kukabidhiwa cheti maalumu

Zaidi ya Makada 800 wa Chama cha Mapinduzi wamepata mafunzo maalumu ambayo ni sehemu ya mpango mkakati wa chama hicho kujiimarisha kisiasa na kusimamia serikali kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa misingi imara na demokrasia yenye tija kwa umma.

Mafunzo ya awali yalifanyika mwanzoni mwa mwezi septemba katika Chuo cha Ihemi Iringa na awamu ya pili yamekamilika leo katika Chuo cha Vijana Tunguu Zanzibar ambapo makada walioteuliwa wamepewa uwezo na nyenzo za ufundishaji watakazotumia kutoa mafunzo kama hayo kwa makada katika ngazi za Shina, Tawi na Kata nchi nzima

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *