Balozi Sirro Atinga Madarasani Kigoma abaini utoa na kutoa somo

Na. Fadhili Abdallah,

RUJAT, Kigoma

WALIMU wa shule za msingi katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wamesema kuwa wazazi wasiosimamia maendeleo ya elimu ya watoto wao wamekuwa changamoto kubwa katika matokeo yasiyoridhisha ya kielimu katika shule hizo.

Walimu hao walisema hayo wakati Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro alipofanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya shule za msingi katika manispaa ya Kigoma Ujiji ikiwa ni siku chache baada ya matokeo ya mitihani ya Taifa ya darasa la saba.

Katika shule ya Msingi Bushabani Mwalim Mkuu wa shule hiyo, Ramadhan Thabiti alisema kuwa shule hiyo kwa sasa ina wanafunzi wengi ikiwa na wanafunzi Zaidi ya 2000 shule ikikabiliwa na idadi kubwa ya utoro kwa wanafunzi na walipofuatilia waligundua wanafunzi wengi wanalelewa na mzazi mmoja au kulelewa na bibi wakati wazazi wakiishi maeneo mengine.

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro Balozi Sirro akizungumza na walimu na wanafunzi alipofanya ziara katika baadhi ya shule za msingi za manispaa ya kigoma Ujiji baada ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba.
Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro Balozi Sirro akizungumza na walimu na wanafunzi alipofanya ziara katika baadhi ya shule za msingi za manispaa ya kigoma Ujiji baada ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba.

Mwalim Thabiti alisema kuwa licha ya hali hiyo wazazi wengi au walezi wa wanafunzi hao wamekuwa hawafiki shuleni wanapoombwa kufanya hivyo kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao au kujadili mipango mbalimbali ya maendeleo ya shule.

Kwa upande wake Mwalim Mkuu wa shule ya Msingi Rasini, Ndaha Seleman alisema kuwa wazazi wanaoshindwa kusimamia watoto wao wanachangia shule hiyo kufanya vibaya kwani watoto wanakaa nyumbani muda mrefu na kuja shule wakati wa mitihani na shule ikikataa kuruhusu watoto hao kufanya mitihani wazazi wanalalamika.

Also Read  Jeshi la Zima moto na uokoaji latoa mafunzo kwa vijana mkoani Iringa

Naye Mwalim Hadija Mwamba alisema kuwa wazazi wamekuwa hawajitokezi kwenye vikao shule vinavyozungumzia nidhamu za watoto wao mipango ya maendeleo ya shule hivyo inakuwa ngumu kwa baadhi ya maamuzi kutekelezwa vizuri kwani wazazi wamekuwa wakilalamikia maamuzi ambayo shule inafanya.

Kufuatia taarifa hizi MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka walimu wakuu wa shule za msingi, Kamati za shule na ofisi za watendaji wa mitaa na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi ambao wamekuwa kichocheo cha utoro sugu kwa watoto wao.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sheria ya elimu inafafanua namna shule na kamati za shule zinavyoweza kuchukua hatua kwa wazazi wazembe wanaoshindwa kusimamia elimu ya watoto wao ikiwemo kwa watoto wasiohudhuria masomo hivyo lazima sheria hiyo ifanye kazi kwa wazazi wazembe. wanaosbabisha utoro sugu ambao unachangia pia ufaulu duni wa wanafunzi.

Pamoja na hilo Mkuu huyo wa mkoa Kigoma aliwapongeza walimu wa shule za msingi mkoa Kigoma kwa kuufanya mkoa huo kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa la saba akieleza kuwa serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza ikiwemo uhaba wa walimu, vitendea kazi na motisha kwa walimu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *