Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, madereva walielezea kwa kina kiini cha mgomo sambamba na changamoto wanazokabiliana nazo katika kazi zao huku nyingi zikiwa ni lawama na tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini LATRA
Baada ya majadiliano ya kina baina ya serikali na madereva hao, viongozi kwa pamoja wamekubali kusitisha mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili, hatua inayowezesha huduma za usafiri kuendelea kama kawaida.
Aidha, Serikali imeeleza utayari wake wa kusikiliza na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva, kwa lengo la kupata suluhisho la masuala yaliyosababisha mgomo huo.

Miongoni mwa kero zilizosababisha mg0mo huo ambao ulisababisha usubufu kwa maelfu ya wasariri nchi nzima ni pamoja na Ukamataji holela wa polisi, ukataji wa point kwenye leseni za madereva wanaokutwa na makosa ya usalama barabarani, ufungiwaji wa leseni, kufanyishwa mitihani na LATRA na changamoto za ubovu wa barabara katika baadhi ya maeneo nchini.
Mhe. Mwigulu Nchemba serikali itaendelea kuhakikisha huduma za usafiri zinaendelea kutolewa huku majadiliano kuhusu changamoto za madereva yakiendelea kati ya Serikali na wadau husika.






