RC Iringa ahimiza jamii kushiriki maonesho ya wiki ya utafiti kwa tija

Na. Hafidhi Ally – RUJAT Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewataka wananchi  kutumia fursa ya Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Huduma kwa Jamii kujifunza na kunufaika na tafiti mbalimbali zinazolenga kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mh. Kheri amesema kuwa Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 2 hadi 4, 2026 katika viwanja vya Bustani mjini Iringa, yakihusisha taasisi za utafiti, vyuo pamoja na wabunifu kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kupitia Maanesho hayo wananchi watapata fursa ya kuona miradi mbalimbali iliyotekelezwa kutokana na utafiti uliofanywa na watafiti Mkoani Hapa.

Ndugu Selina Mkimbili Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Selina Mkimbili, amesema baadhi ya tafiti zitakazooneshwa zinahusu zao la ulanzi pamoja na uyoga unaozalishwa mkoani Iringa.

Tafiti hizo zinalenga kuongeza thamani ya mazao hayo pamoja na kuwasaidia wananchi kutumia mbinu bora za uzalishaji na uhifadhi ili kuongeza kipato na tija katika sekta ya kilimo.

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa mitano nchini yenye kiwango cha juu cha uzalishaji wa mazao ya kilimo na misitu ikiwemo miti, mbao na mahindi.

About The Author

Also Read  Ushirika watajwa kuwa chachu ya maendeleo mkoani Kigoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *