Kheri James atoa maagizo mazito Mufindi-ataka uwajibikaji

Na. Hafidhi Ally, RUJAT Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ameizagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika mwaka wa fedha 2024/2025 ili kuongeza uwajibikaji na usimamizi mzuri.

Mh. Kheri ameyasema hayo wakati wa Baraza Maalumu la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi la kujadili Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, ambapo pamoja na kupata hati safi, halmashauri hiyo ilipitia hoja 64 zilizowasilishwa katika ripoti hiyo.

Mh. Kheri James amesema kuwa ni vyema baraza hilo likaweka utaratibu wa kukutana na wataalamu kueleza wanavyotekeleza majukumu yao kwani kutofanya hivyo kutapelekea baraza hilo kuvunjwa.

Aidha Mh. Kheri James amewataka viongozi wa halmashauri kuendelea kuimarisha mifumo ya ukusaji wa mapato ili waweze kufikia lengo la kukusanya Bilion 10.3 katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Kwa upande wao, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa, Mwenyekiti wa Halmashauri Castory Masangula, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Mashaka Mfaume, wamemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili kuendelea kuboresha utendaji na kuimarisha maendeleo ya Wilaya ya Mufindi.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha na kushughulikia kwa wakati hoja zilizobainishwa ili kudumisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

About The Author

Also Read  Serikali yazindua proramu ya kuimarisha uongozi shule za Sekondari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *