Samizi aipiga tafu shule ya sekondari Malagarasi -Kibondo

Naibu Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Wilayani Kibondo mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi, amekabidhi mifuko 209 ya saruji katika shule ya Secondari Maragalasi, ikiwa ni muendelezo wake wa kuisapoti Shule hiyo ambayo inajenga Fensi ili kuifanya shule hiyo kuwa na mazingira rafiki kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Akikabidhi nyenzo hizo za ujenzi, Dkt. Samizi, amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshaweka miundombino bora inayoifanya shule hiyo kuwa na mazingira rafiki kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, akiwaeleza kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa walimu katika Taifa letu la Tz.

Shehena ya saruji iliyokabidhiwa kwa shule ya sekondari Malagarasi wilayani Kibondo katika jimbo la Muhambwe

Wilaya ya Kibondo, iliyopo mkoani Kigoma, ina jumla ya shule za sekondari 32. Kati ya hizi, 24 ni za serikali na 8 ni za binafsi. Shule hizi zimesambaa katika kata 13 za wilaya, ikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha kila kata inakuwa na angalau shule moja ya sekondari kupitia mpango wa jamii kujenga shule (Community Based Program).

Kati ya shule hizi, 20 ni za sekondari za awali (O-level) na shule mbili 2 ni za upili pkee (A-level)  na shule mbili (2) zinatoa elimu ya O-level na A-level.

Shule zinazotoa elimu ya sekondari hadi kidato cha 6 A-level ni pamoja na Kibondo Girls’ Secondary School, Mkugwa Girls’ Secondary School, Malagarasi Secondary School, na Boniconsilii Mabamba Secondary School.

About The Author

Also Read  Polisi Mkoani Iringa yawacharukia makampuni binafsi ya Ulinzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *