Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladmir Putin katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladmir Putin mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow Nchini Urusi, tarehe 03 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati alipowasili katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow Nchini Urusi, tarehe 03 Juni, 2026.

Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan akiingia ndani ya Ikulu ya Urusi tayari kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Putin

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladmir Putin katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow Nchini Urusi, tarehe 03 Juni, 2026.

Shada la maua maalumu kwa ajili ya mashujaa wa Urusi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Shada la maua kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati alipokuwa akiondoka katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow Nchini Urusi, tarehe 03 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladmir Putin mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow Nchini Urusi, tarehe 03 Juni, 2026.






