Na. Konstebo Abdulkarim Adam, Kigoma
Ofisi ya Uhamiaji Kanda Maalumu Mkoa wa Kigoma imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 95 katika muendelezo wa operesheni maalum za kudhibiti uhamiaji usio halali mkoani humo.
Akizungumza mapema leo kuhusu tukio hilo, Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma, ACI Jeremiah Mwakibinga, amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao wanatoka katika mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watuhumiwa walikamatwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba za kulala wageni, stendi ya mabasi pamoja na kumbi za starehe zilizopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara moja Kwa kosa la kuingia Nchini kinyume Cha Sheria.
ACI Mwakibinga amewasisitiza wananchi Kupitia Kampeni ya Uhamiaji ya MJUE JIRANI YAKO kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini uwepo wa watu wanaoshukiwa kuingia au kuishi nchini kinyume cha sheria Ili kuendelea Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Taifa.
#UhamiajiUsalamaNaMaendeleo*
#MjueJiraniYako*






