Halmashauri Kigoma zahimizwa kulinda Malikale

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Mwenyekiti wa Taasisi ya Ujiji Heritage & Development (UHDO),Shekhe Hassan Kabeke amezitaka Mamlaka za Serikali za mitaa na serikali kuu kuyatambua,kuyahifadhi na kuyalinda maeneo mbalimbali ya kihistoria ambayo kwa sasa yameanza kupotea kutoka na taratibu za ujenzi zinazoendelea.

Shekhe Kabeke ambaye ni Shekhe wa mkoa Mwanza alisema hayo akitoa salamu za taasisi hiyo kwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid wakati wa Tamsha la Utamaduni la Ujiji lililofanyika kwenye uwanja wa Kawawa Ujiji Mjini Kigoma.

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mussa Maulid akizungumza katika Tamsha la utamduni la Ujiji linalofanyika Ujiji mjini Kigoma

Katika hilo aliyataja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na aliyofikia Baba wa Taifa Marehemu Mwalim Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru, maeneo aliyotumia kukutana na watu, sehemu za kihistoria za nyumba na maeneo yaliyotumiwa na waarabu wakati wa enzi za utumwa na wageni Wamisionari mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Karuta ambavyo kwa sasa historia yake inapotea.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Ujiji Heritage & Development Organization (UHDO) Shekhe Hassan Kabeke akizungumza katika tamasha la utamaduni la Ujiji lililofanyika Ujiji mjini Kigoma Juni 21 mwaka huu

Aidha katika salamu zake Shekhe Kabeke alionya mmonyoko mkubwa wa maadili unaotokea Kigoma kutokana na kuachwa kwa mila,desturi na tamaduni za malezi na makuzi ya vijana hivyo kuwepo kwa mambo yasiyofaa ikiwemo kuwepo kwa mambo ya ushoga.

Akizungumza katika Tamasha hilo Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji , Mussa Maulid alisema kuwa maeneo yenye historia ya uhuru wetu, safari za wageni mbalimbali wakiwemo waarabu na wamisionari yanapaswa kulindwa na kutunzwa hivyo atalifikisha kwenye mamlaka za halmashauri ili lifanyiwe kazi kwa vitendo.

Also Read  Trilion 1.2 zimetumika, Watumishi 5000 wa kada ya afya wameajiriwa- Dkt. Samizi

Pamoja na hilo Meya Maulid ameitaka idara ya uhamiaji kutumia sheria na busara katika kushughulikia masuala ya watu wanaokamatwa kwa changamoto za uraia kwani baadhi ya matukio yanayofanywa na uhamiaji yanakiuka mila, tamaduni za mkoa Kigoma na kutenganisha familia .

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *