TRA Kigoma yatangaza neema kwa Wafanyabiashara Wadogo

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kigoma inatarajia kuja na mpango mkakati maalumu unaolenga kuinua wafanyabiashara wadogo ili kukuza biashara zao na hatimaye kuingia kwenye mfumo rasmi wa ulipaji kodi.

Meneja wa TRA Mkoa wa Kigoma, Beatus Nchota, alisema hayo akikabidhi ssamani za ofisi kwa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) Halmashauri ya wilaya Kigoma mkoani Kigoma na kueleza kuwa elimu ya biashara itakuwa nyenzo kuu ya kufanikisha mpango huo unaotarajia kuanza Julai Mosi mwaka huu.

Akizungumza na wafaanyabiashara hao Nchota alisema kuwa mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wana uwezo wa kukuza biashara zao lakini wanakabiliwa na changamoto za uelewa wa masuala ya usimamizi wa biashara, utunzaji wa kumbukumbu za mapato na matumizi pamoja na fursa za masoko.

Meneja wa TRA Mkoa wa Kigoma, Beatus Nchota akizungumza na wajasiriamali Kigoma

“Lengo letu si kukusanya kodi pekee, bali pia kuona wafanyabiashara wanakua kiuchumi. Tunapotumia elimu ya biashara kuwajengea uwezo, tunawawezesha kuongeza mauzo, kupata faida zaidi na hatimaye kuingia kwenye wigo wa ulipaji kodi kwa hiari,” alisema Nchota.

Akizungumzia msaada wa samani uliotolewa kwa Shirikisho hilo la Umoja wa Machinga Meneja huyo wa TRA alisema kuwa unalenga kuwatia moyo na kuwaunga mkono ili biashara zao zikue na kuweza kulipa kodi Zaidi kwa biashara wanazofanya kwani hata sasa wanaponunua bidhaa hizo na kuja kuuza pia zimekuwa zikikatwa kodi.

Meneja wa TRA Kigoma Beatus Nchota akikata utepe wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa wajasiriamali

Wakizungumza baada ya kupokea samani hizo viongozi wa SHIUMA Halmashauri ya wilaya Kigoma akiwemo Mwenyekiti wa Umoja huo, Zuwena Hussein alisema kuwa kwa sasa TRA imekuwa ikifanya kazi kama mshirika kwa kusikiliza changamoto za biashara wanapokuja kwenye biashara zao badala ya kuwa taasisi ya usimamizi pekee si kama ilivyokuwa hapo awali jambo linalochangia wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari na kuwepo kwa ongezeko la walipa kodi wapya.

Also Read  Muhimbili mpya kwa wagonjwa inakuja - Mchengerwa

Zuwena alisema kuwa anaamini mpango huo wa kukuza wafanyabiashara wadogo utakuwa na manufaa makubwa kwao kwani wanatamani kufika huko lakini elimu duni ya biashara na elimu yaa kodi imkuwa kikwazo na kuwafanya kutoua njia ya kupita kupataa mafanikio.

Akisoma risala kwa viongozi wa TRA Katibu wa SHIUMA Halmashauri ya wilaya Kigoma, Moshi Ramadhani alisema alisema kuwa kutolewa kwa samani hizo kutaunga mkono utekelezaji wenye tija wa shughuli zao na kuchangia ukuaji wa biashara zao na kuwa walipa kodi wapya ambao watalipa kodi kwa hiari.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *