REA yaingia sabasaba na mtindo wa elimu kwa umma

Mwandishi wetu, Dar es salaam

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeanza kutoa elimu kwa wananchi wanaoshiriki na kutembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo yameanza Juni 28, 2026 na yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 13, 2026.

Katika banda la REA, wananchi wanapata fursa ya kuelimishwa kuhusu miradi ya umeme inayotekelezwa katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji, pamoja na utekelezaji wa miradi ya nishati safi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo hayo.

REA imewahimiza wadau na wananchi kutembelea banda lake ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu miradi inayoendelea kutekelezwa na huduma zinazotolewa na wakala huo.

Kaulimbiu ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026 ni: “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania.”

About The Author

Also Read  Wahamiaji 95 wasio na vibali wakamatwa mkoani Kigoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *