Nipo tayari kwenda Mahakamani kupambana – Mh. Katambi

  • Kufungua kesi Mahakamani ni Hasira ya Kufeli Maandamano

Na. Abubakar Akida, Shinysnga

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Katambi amesema hatokua tayari kuona kundi la watu wachache wenye maslahi binafsi wanachezea amani iliyopo kwa kujificha katika kichaka cha Haaki za binadamu na Demokrasia huku akiwahakikishia jamii ya watanzania kuendelea kuwepo kwa Hali ya Utulivu nchini huku akisema yupo tayari kwenda mahakamani hata usiku ili jamii iweze kupata suluhu ya Wapotoshaji wanaotumika kuchochea chuki na kuhatarisha amani ya Nchi kwa maslahi yao binafsi na kundi.

Ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti akizungumza Makundi ya Walinzi wa amani katika jamii, Polisi jamii, Wazee, Sungusungu, Wenyeviti wa Mitaa,Mabalozi na Wenyeviti wa Vitongoji Vitongoji,Shinyanga Mjini.

“Wanajua wakiichafua Tanzania yetu amani ikapotea tutapoteza mvuto kwa watalii,Nchi iwekewe vikwazo, Miradi mikubwa ya maendeleo itasiama,kubomoa mahusiano ya kidiplomasia, kutisha wawekezaji, tutapoteza mapato ya bandari ambapo timu hiyo inayosema inanipeleka mahakamani ndiyo hiyo hiyo ilikua inapinga Mkataba wa Uwekezaji wa bandari lakini sasa hivi bandari inaingiza fedha nyingi sana na tumeanza kwenda mbele ikiwa ni hatua za Taifa kuanza kujitegemea,wameshindwa kuwapeleka mahakamani ambao wanachochea kuangamiza Taifa letu kwa kuchoma moto,zichomwe moto shule,vituo vya mafuta,ofisi za serikali,mali na biashara za watu binafsi zichomwemoto,wavamie vituo vya polisi. Kama wanauchungu kweli na haki za Binadamu ni lini na wapi mliwasikia wanakemea vitendo hivyo hatarishi kwa uhai wa watu na Taifa?” amesema Waziri Katambi

“Wanachochea fujo lakini watoto wao,wake zao wako nje ya nchi, wanatembea na Pasport za kusafiria mfukoni,leo hii yakitokea machafuko wazee wangu mtaenda wapi? watoto, wanawake na wenyeulemavu si ndio wahanga mmewafikiria? Nchi yetu ni Tanzania hamna nchi nyingine,kuna nchi za Burundi,Rwanda na Kongo yalitokea machafuko tumehifadhi Wakimbizi kwa miaka mingi kutoka nchi hizo je wanataka na sisi tukawe wakimbizi? Mimi Katambi hilo siwezi kukubali litokee tumepewa dhamana ya kulinda amani ya nchi hii kwa viapo tutailinda kwa gharama zote.” aliongeza Waziri Katambi

Also Read  Joto la SGR lapanda Kasulu, Halmashauri kunufaika

Amesema bado hajapokea wito wa kuitwa mahakamani lakini yuko tayari kwenda huko hata usiku wa manane akipokea wito huku akisisitiza mahakama ndio chombo pekee Huru na chenye mamlaka ya kusema Katiba imevunjwa na sio jukumu la mtu au taasisi fulani kusema Katiba imevunjwa hawana mamlaka wala usahihi huo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *