“Marali” ya wananchi Ilongole yatumika kuhimiza mradi wa maji Mafinga

Wananchi wa Mtaa wa Ihongole, Halmashauri ya Mji Mafinga, wamejitolea kuchimba mtaro na kupokea vifaa kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji unaosimamiwa na Shirika la People Development Forum (PDF), kwa lengo la kusambaza huduma ya maji ya bomba katika eneo hilo.

Wakizungumza wakati wa kushiriki shughuli hiyo ya maendeleo inayolenga kufikisha huduma ya maji katika Shule ya Msingi Mwongozo, baadhi ya wananchi wamesema wameamua kujitolea kuchimba mtaro ili kurahisisha uwekaji wa mabomba na hatimaye huduma ya maji kuwafikia wananchi na wanafunzi.

Wananchi wa Kata ya Boma wakitoa nguvu kazi kuhakikisha mradi wa maji unakamilika

Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Mwongozo, Atu Mng’ong’o, amewashukuru wazazi na wananchi kwa kujitolea kufanya kazi za mikono, akisema hatua hiyo itarahisisha huduma ya maji kufika shuleni hapo na kupunguza changamoto ya wanafunzi kufuata maji wakati wa masomo.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Boma, Baraka Kisakanike, amesema mradi huo utasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Mtaa wa Ihongole.

Bw. Baraka Kisakanike  Diwani wa kata ya ya Boma, Halmashauri ya Mji Mafinga

Aidha, Diwani Kisakanike amesema huduma hiyo itawanufaisha wananchi wa kata hiyo, huku akilishukuru Shirika la People Development Forum (PDF) pamoja na Serikali kwa kushirikiana katika utekelezaji wa mradi huo.

Wananchi wa Kata ya Boma wakichimba mtaro kwa ajili ya kuitandaza bomba

About The Author

Also Read  Mbegu bora ni nyezo mhimu ya mafanikio kwa wakulima- RC Iringa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *