Pelekeni huduma maeneo yenye uhitaji mkubwa, DC Mfundi azitaka NGO

Na. Hafidhi Ally, Iringa

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi ya maendeleo Wilayani Mufindi kupeleka miradi ya maendeleo katika maeneo yenye uhitaji zaidi.

Dkt Linda ameyasema hayo katika Jukwaa la Mashirika yasiyo ya kisekali NACONGO lililofanyika katika ukumbi wa Mbalamaziwa Wilayani Mufindi na kuongeza kuwa serikali inatambua mchango wa mashirika hayo huku akisisitiza ni vyema miradi ya maendeleo kama maji, elimu na afya ikaelekezwa zaidi katika maeneo ambayo yana hizo changamoto.

Amesema kuwa Mashirika hayo yamekuwa yakifanya kazi kubwa ya kusaidia serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora maeneo yote.

Kwa upande wake Zacharia Shibukulu kutoka  Shirika la World Visson Wilaya ya Mufindi amesema kuwa shirika lao limekuwa na mkakati wa kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yenye uhitaji jambo ambalo limepelekea kuwafikia wananchi wengi kupitia miradi ya afya, elimu, kilimo na ufugaji.

Amesema kuwa shirika hilo kwa sasa linahudumia nchi zaidi ya Mia moja ulimwenguni kote katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali za kimaendeleo.

Naye mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NACONGO Wilaya ya Mufindi, Phideli Filipatali alisema kuwa Kupitia umoja wa mashirika hayo, wameweka azma ya kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akiunga mkono hoja ya Mkuu wa Wilaya Linda Salekwa ya kupeleka miradi hiyo katika maeneo yenye uhitaji zaidi.

About The Author

Also Read  Wananchi Kalenga-Iringa wakerwa na uchakavu wa barabara, Mbunge atoa hoja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *