RUJAT na Idara ya Habari “Maelezo” wakubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati

Na Hamida Ramadhan, RUJAT – Dodoma

CHAMA cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT) kimefanya ziara ya kikazi katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mtumba jijini Dodoma, kwa lengo la kujitambulisha rasmi na kujenga ushirikiano utakaosaidia kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari nchini.

Ujumbe wa RUJAT uliongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Neville Meena, akifuatana na Katibu, Prosper Kwigize, Zena Mohammed ambaye ni Mhasibu wa chama pamoja na mjumbe wa Kamati Tendaji Hamida Ramadhan kutoka kanda ya Kati Dodoma.

Katika ziara hiyo, viongozi hao walikutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO)

, Kelvin Kanje, ambapo walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya wizara na RUJAT katika kukuza taaluma ya uandishi wa habari, hususan kwa waandishi wanaofanya kazi katika maeneo ya vijijini.

Akizungumza katika kikao hicho, Kinje aliukaribisha uongozi wa RUJAT na kupongeza kuanzishwa kwa chama hicho pamoja na kushukuru kwa kufika wizarani kujitambulisha na kujadili masuala ya kisekta.

Alisema wizara ipo tayari kushirikiana na RUJAT katika masuala mbalimbali ya kitaaluma na yasiyo ya kitaaluma yatakayosaidia kukuza sekta ya habari nchini hususani kuhakikisha habari za vijijini zinaandikwa, kuchapishwa na kutangazwa.

Bw. Kanje aliweka bayana kuhusu wajibu wa Idara ya Habari (Maelezo) katika kuhakikisha waandishi wa habari wanapata taarifa sasahihi kutoka serikalini pamoja na taasisi zake na kwamba Ofisi yake iko tayari kuanzisha ushirikiano wa kimkakati katika masuala mbalimbali ya ujenzi wa uwezo wa wanachama wake kwa maslahi ya Taifa.

Aidha, aliwasisitiza wanachama wa RUJAT kuhakikisha wanamiliki ithibati za uandishi wa habari, akieleza kuwa ithibati hizo ni utambulisho rasmi wa mwandishi wa habari na humwezesha kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na maadili ya taaluma hiyo.

Also Read  Mkurugenzi REA atoa mwongozo kwa watumishi kutimiza wajibu kwa weledi

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa RUJAT, Neville Meena, alisema chama hicho kimejipanga kuendelea kujenga mahusiano mazuri na taasisi za Serikali pamoja na wadau wa sekta ya habari ili kuongeza uwezo wa waandishi wa habari, hususan waliopo vijijini, na kuwapa fursa zaidi za mafunzo na maendeleo ya taaluma.

Naye Katibu wa RUJAT, Prosper Kwigize, alisema ushirikiano na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo utasaidia chama hicho kutekeleza malengo yake ya kukuza uandishi wa habari wenye weledi, kuimarisha maadili ya taaluma na kuhakikisha waandishi wa habari vijijini wanapata mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao.

Aliongeza kuwa RUJAT itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kutetea maslahi ya waandishi wa habari na kuchangia maendeleo ya sekta ya habari nchini kupitia katika ujenzi wa uwezo wa wanachama kitaaluma pamoja na kuwaunganisha waandishi wa habari na fursa mbalimbali zinazopatikana ikiwemo kuwahakikisha usalama kazini na katika jamii.

Wakati huo huo; Bodi ya mfumo wa stakabadhi za ghala WRRB imeahidi kushirikiana na RUJAT katika kutangaza taarifa na habari zinazohusu mfumo wa stakabadhi za ghala na fursa zinazotokana usimamizi bora wa maslahi ya wazalishaji na wafanyabiashara za mazao nchini.

Ndugu Asangye Bangu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani (WRRB)

Akiongea na viongozi wa RUJAT muda mfupi baada ya mkutano na waandishi wa habari wa mkoani Dodoma, Murugenzi wa bodi ya usimamizi wa mfumo wa stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu aliihakikishia RUJAT kuwa Bodi iko tayari kuanzisha ushirikiano wa kihabari utakaowezeha wananchi kuuifahamu mfumo wa stakabadhi na namna unavyochangia katika ukuaji wa uchumi wa wakulima na taifa.

Also Read  Muhimbili mpya kwa wagonjwa inakuja - Mchengerwa
Bw. Prosper Kwigize Katibu wa RUJAT (kushoto nyuma) akisikiliza kwa umakini maelezo ya Mkurugenzi wa bodi akielezea kuhusu majukumu na matokeo ya kazi za Bodi ya mfuko wa stakabadhi za ghala

Bw. Bangu aliialika RUJAT kuendeleza mawasiliano na ofisi yake ili kupanua wigo wa mjadala wa nini kinapaswa kufanyika ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari kufahamu mfumo na wajibu wa Bodi ya stakadhadhi za Ghala nchini

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *