Askari Polisi Kakonko atoa semina kwa wakulima shambani

Na. Mwandishiwetu -Kakonko

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limewataka wazazi na walezi katika Kata ya Nyabibuye, Wilaya ya Kakonko, kuhakikisha watoto wanapewa kipaumbele cha masomo kabla ya kushiriki katika shughuli za kilimo, hususan kipindi hiki cha mavuno.

Rai hiyo imetolewa Aprili 30, 2026 na Mkaguzi wa Polisi (INSP) Meshack Elia alipokuwa akitoa elimu kwa wazazi na watoto waliokutwa mashambani wakijihusisha na shughuli za mavuno.

Amesisitiza kuwa, licha ya umuhimu wa kazi za shamba, watoto wanapaswa kuhudhuria masomo yao kikamilifu na kushiriki kazi hizo baada ya kurejea nyumbani jioni.

Aidha, INSP Meshack amewahimiza wananchi wa eneo hilo kuepuka vitendo vya wizi wa mazao na kuhakikisha kila mmoja anavuna katika shamba lake halali.

Katika hatua nyingine, amewataka wananchi kuendelea kuheshimu sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi, akisisitiza kuwa amani na utulivu ni msingi muhimu wa maendeleo ya jamii.

About The Author

Also Read  TANESCO yapeleka shangwe Lindi na Mtwara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *