TRA yatoa cheti cha pongezi kwa “Boss” mamlaka ya uagizaji mafuta

Na. Mwandishi wetu – Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Bw. Erasto Simon, amepokea Cheti cha Shukrani na pongezi kutoka kwa Mamlaka ya mapato Tanzania kama sehemu ya kutambua mchango wa mamlaka hayo.

Cheti hicho kimekabidhiwa kwake na Naibu Kamisha wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Wahabi Matengo, akieleza kuwa cheti hicho ni kwa ajili ya kutambua mchango na juhudi za taasisi hiyo katika kuhakikisha upatikanaji salama wa mafuta pamoja na uwepo wa bei shindani nchini.

Akikabidhi cheti hicho leo tarehe 13 Mei, 2026, Bw. Matengo ameipongeza PBPA kwa kuendelea kusimamia kwa ufanisi mchakato wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja, hatua ambayo imeendelea kuisaidia Serikali kuongeza mapato kupitia ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali.

Kwa upande wake, Bw. Erasto Simon amesema PBPA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unaendelea kuwa wa uhakika, salama na wenye kuwanufaisha wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla.

Amesema mafanikio hayo yanatokana na maboresho ya mifumo ya usimamizi wa mafuta, matumizi ya teknolojia za kisasa pamoja na ushirikiano mzuri kati ya Serikali na wadau wa sekta hiyo.

About The Author

Also Read  INEC yateua wagombea Uchaguzi jimbo la isimani,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *