Mafinga yavuka lengo kabla ya muda, ukusanyaji wa mapato

Na. Hafidh Ally – Iringa

Halmashauri ya Mji mafinga imefanikiwa kuvuka lengo la kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 105 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2025/2026.

Hayo yamebainishwa leo katika kikaoo cha Baraza la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Mafinga ambacho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa wa Iringa

Akizungumza katika cha Kikao cha Baraza la Madiwani Halmshauri ya Mji Mafinga kutoa tathmini ya Robo tatu ya mwaka 2025/2026, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo  Bw. Reginant Kivinge amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano baina ya madiwani na wakuu wa idara kwa kufanya kazi kwa weledi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Bi Fidelica Myovella amebainisha kuwa Halmashauri hiyo itazidi kufuata maelekezo ya serikali ikiwemo kujibu hoja na masuala ya ufungaji wa hesabu ili kuendeleza kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.

Baadhi ya Madiwani wakishiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani

Naye Afisa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Sifael Kivamba ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuvuka lengo la kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani huku akiwataka kuendeleza mkazo huo katika mwaka ujao wa fedha.

Halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi Bilion 8.8 na kufanikiwa kuvuka lengo kwa asilimia 105 ya makusanyo ambayo walikadiria kukusanya shilingi Bilion 7.5.

 

About The Author

Also Read  Dkt. Samia azuru gereza la Ukonga, kituo cha urekebishaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *