Athari za kimazingira maeneo ya wakimbizi kushughulikiwa

Na. Mwandishi wetu – Kibondo

Serikali kupitia mfuko wa Dunia wa mabadiliko ya tabia nchi  (GCF) wameanza hatua za awali za kurekebisha mazingira katika maeneo yaliyokuwa yakihifadhi wakimbizi nchini Tanzania kama sehemu ya mpoango wa dunia wa kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi

Chini ya mpango huo shughuli zilizoainishwa ni pamoja na kupanda miti na kuhamasisha  kilimo mseto  katika maeneo ambayo yameathiriwa na shughuli za huduma kwa wakimbizi ili kuwajengea uwezo wananchi wa vijiji vya Jirani za zilizokuwa kambi kutumia ardhi na misitu kwa tija na kurejesha uoto asilia.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa kambi za Nduta, Mtendeli na Nyarugusu, Mkuu wa wilaya ya kasulu kanal Isack Mwakisu aliyefuatana na maafisa kutoka ofisi ya Makamu wa Rais kitengo cha Mazingira amebainisha kuwa Serikali pamoja na GCF wamekaa kikao kazi  amacho kimelenga kuthibitisha  vigezo vya kuchagua maeneo kwa ajili ya usimamizi shirikishi wa mistu ya jamii katika zilizokuwa kambi za wakimbizi na maeneo mengine.

Mkuu wa Wialaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu akizungumza na wadau na kutoa hakikisho la usalama

Kanali Mwakisu amewahakikishia maafisa wa Umoja wa Mataifa ana serikali kuu uwepo wa usalama na  ushirikiano wa kutosha  utakaowezesha taasisi ya utafiti wa misitu Tanzania (TAFORI) ambao ndio watoa ushauri wa kiufundi wa mradi sambamba na ofisi ya makamu wa Rais mazingra ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa ipasavyo kwa manufa ya wananchi.

Aidha Mtafiti kutoka Taasisi ya utafiti Tanzania Daktari Nauman Amanzi pamoja Afisa Mazingra Mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Bw, Isack Emmanuel wamesema katika mradi huo wanakusudia kuwajengea uhimilivu wananchi wa wilaya za kasulu, kakonko na kibondo juu ya athali za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yametokana na uwepo wa shuguli za wakimbizi.

Also Read  ILO yawafunda waandishi wa habari kuhusu masuala ya Uhamiaji

Kwa upande wao wataalamu wa idara mbali mbali kutoka katika wilaya hizo ambao wameshiriki kikao kazi hicho  mmoja wao akiwa Bi Dorisia Kashoa  wamesema mradi huo ambao umelenga kuwajengea uwezo wananchi juu ya namuna ya kukabiliana na mabadiiko ya tabia nchi utasaidia sana kuondokana na maeneo mengi kuwa jangwa na kurejesha uoto wa asili.

Mradi huu wa miaka mitano unaotekelezwa na wilaya ya Kibondo, Kakoko, Kasulu kwa kushirikiana na TFS utatekelezwa katika vijiji 22 vya wilaya hizo ikiwa ni mkakati  wa serikali wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo hayo ambaayo yanazungukwa na kambi za wakimbizi .

Mkoa wa Kigoma unahifadhi wakimbizi takribani 100,000 wengi wao wakitoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wachache kutoka Jamhuri ya Burundi na wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.

Picha ya pamoja ya wadau uwa mazingira, viongozi wa serikali na maafisa kutoka GCF baada ya kujadiliana kuhusu utekelezaji wa mradi huo

Kambi za Mtendeli na Nduta tayari zimefungwa na wakimbizi wengi walirejea nchini Burundi kabla ya wachache waliosalia kuhamishiwa katika kambi ya Nyarugusu kutokana na sababu mbalimbali na wachache wako katika kituo cha NMC Kigoma kwa ajili ya uangalizi maalumu na kutatua changamoto zao ambazo huenda zikawalazimu kupata hifadhi nchi ya tatu badala ya kurejea nchini Burundi.

Mkoa wa Kigoma, Tabora, Katavi na Kagera imekuwa mwenyeji wa maelfu ya wakimbizi kutoka nchi za Burundi, DRC, Rwanda na wachache kutoka Sudan, Somalia na Kenya tangu mwaka 1962 ambapo kambi nyingine ziligauka kuwa makazi hususani Katumba, Mwese na Mishamo mkoani Katavi, Ulyankuru mkoani Tabora, huku kambi nyingine za mkoani Kagera ikiwemo Lukole kufungwa na wakimbizi kurejea katika nchi zao.

Also Read  TANESCO yapeleka shangwe Lindi na Mtwara

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *