Kakonko yatoa tuzo nzito kwa washindi katika pambano la SHIMISEMITA Mbeya

Na. Meandishi wetu, Kakonko

Wachezaji wa timu ya Basketball ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko walioshika nafasi ya kwanza katika mashindano ya SHIMISEMITA yaliyofanyika Mbeya, wamezawadiwa hati ya kiwanja kilichopimwa kila mmoja katika eneo la Mganza kwa kutambua mchango wao katika kuiletea Halmashauri ushindi.

Zawadi hiyo kwa kila mchezaji ni sehemu ya kutambua juhudi, nidhamu na mshikamano walioonesha katika kuiwakilisha Halmashauri, ambapo timu ya mpira wa kikapu imeibuka mshindi wa kwanza kitaifa na kukabidhiwa kombe la mshindi wa kwanza katika mashindano huku timu hiyo ikikabidhi kombe hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Col. Evance Mallasa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Ndaki Stephano Mhuli.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Col. Evance Mallasa aliwapongeza wachezaji kwa ushindi huo na kuwataka kuendeleza umoja na mshikamano waliouonesha katika michezo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri, Ndaki Stephano Mhuli ameeleza kuwa kutambua mchango wa wachezaji wao na uzalendo wao, Halmashauri imewazawadia kila mchezaji kiwanja kimoja wakiwa jumla ya wachezaji 9 na dereva ambaye alikuwa mhamasishaji mahiri.

Ushindi huo unatarajiwa kuongeza hamasa kwa watumishi kushiriki katika michezo, kujenga afya, mshikamano na kuimarisha utendaji kazi.
#amvano #ikulumawasiliano #TAMISEMI #kigomars #kakonko

About The Author

Also Read  Rais Samia azindua ujenzi wa SGR kutoka Tabora hadi Kigoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *