TANGAZO MHIMU KWA WAANDISHI WA HABARI MIKOA YOTE

Uongozi wa Chama cha waandishi wa habari za Vijijini Nchini Tanzania, tunapenda kuwatangazia waandishi wa habari wanaoandika na kutoa kipaumbele kwa habari za maendeleo vijijini kujiunga na RUJAT ili kuongeza nguvu katika kuandika na kuhabarisha umma kwa ajili ya kusukuma kasi ya maendeleo ya taifa letu

Tunatambua vema kuwa katika maisha ya kijamii na kitaaluma unaweza usijulikane kama upo na unafanya nini mpaka ujiunge na wenzako

Naomba kutambulisha kwako uwepo wa chama cha waandishi wa Habari vijijini “The Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT)” ambacho hadi sasa kina wanachama 120 nchi nzima, unaalikwa wewe na wenzako kujiunga ili unufaike na mengi ikiwemo networking, connections na capacity building zinazotolewa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo serikali,

Pia tunakualika kutuma habari kwa RUJAT ili zichapishwe kwenye tovuti yetu www.rujat.or.tz kutuma habari tumia barua pepe hii rujat.online@gmail.com

Ukitaka kujiunga wasiliana na RUJAT kupitia kwa namba hizi

0653200211 au 0754389048 au 0753555556

Au pakua fomu hii hapa chini isome na kuielewa kabla hujaizaja, kumbuka vigezo na masharti vitazingatiwa kabla fomu yako haijafanyiwa kazi.

Pakua fomu kwa kugusa hapa

Karibu RUJAT CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA VIJIJINI

About The Author

Also Read  Ni Bajeti ya kuimarisha Afya kwa watanzania -Mchengerwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *