Wakulima zabibu walia kutonufaika na zao hilo

Na Mwandishi Wetu – Dodoma

WAKULIMA wa zabibu kutoka vijiji vya Makang’wa na Mvumi Makulu katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wamesema ukosefu wa soko la uhakika wa zao hilo ni sababu ya kutokunufaika na kilimo hicho.

Walisema hayo jana wakati wa mafunzo ya wakulima juu mwongozo wa uzalishaji wa zabibu kwa kanopi yaliyoandaliwa na Shirika la CultivAid yaliyofanyika shamba darasa linalojulikana kama Agricultural Motivation and Technology Centre (AITEC).lililopo Don Bosco Dodoma.

Mkulima kutoka Kijiji cha Mvumi Makulu, Leonard Mangwela alisema kuwa changamoto kubwa ni bei ya zabibu ambayo inasua sua mwaka hadi mwaka,

” Hakuna bei elekezi ya zabibu kutokana na wakulima kutokuwa na umoja linaonekaba kama tunda mwitu,’ alisema

Pia alisema kutokuwa na umoja kwa wakulima kumepelekea kila mtu kukimbizana kivyake.

Alisema kuwa elimu aliyoipata itamsaidia katika kuboresha kilimo chake.

Mkulima mwingine wa zao hilo, Peter Maisel- alisema kuwa bado kuna changamoto kwenye soko la zabibu hasa kwa wakulima waliopo vijijini..

Alisema kutokana na uzalishaji kutokuwa mkubwa wanekuwa wakitegenea wanunuzi wanaofika mashambani.

Pia alisema elimu aliyoipata inamsaidia kuboresha kilimo.

Kwa upande wake,msimamuzi wa shamba la mfano Mvumi Makulu, Alex Mussa alisema kuwa baada ya mafunzo hayo wanategemea mabadiliko makubwa kwenye mashamba ya wakulima na hiyo itaongeza tija kwenye uzalishaji.

” Kwa mafunzo tuliyopata ubora wa matunda ya zabibu utaongezeka,” alisema

Naye, Anna Lubote alisema soko la zabibu bado ni gumu kwani wanaokuja kununua ni wachuuzi.

” Wakija wanachagua wanazozitaka wao nyingine wanakuachia, huwezi hata kuuza tena,” alisema

Pia alisema kama mkulima amejifunza namna ya kufanya matawi ya mzabibu yakae vizuri.

Also Read  Muhimbili mpya kwa wagonjwa inakuja - Mchengerwa

“Tulikuwa hatutoi mapandukizi na mzabibu unakuwa kama msitu,sasa tumejiifunza kukatia mzabibu,” alisema.

Mkurugenzu Mkazi wa CultivAid Eldad Barbar alisema kuwa mafunzo hayo yamewashirikisha wakulima 100, lengo ni kuwapa wakulima elimu na mbinu bora za kisasa katika uzalishaji wa zao la zabibu

Mkurugenz Mkazi wa CultivAid Eldad Barbar alikielekeza wakulima namna bora ya kilimo cha Zabibu

Mchumi wa kilimo kutoka Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Dk Rodgers Lumenyela alisema

Alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakisema wana changamoto kwenye upande wa masoko lakini kinachotakiwa ni kuongeza uzalishaji ili kuwavitia wawekezaji kwani kukiwa na viwanda vya kutosha wakulima watapata soko la uhakika.

Alisema kuwa IRDP na CultivAid wataendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha wakulima wanaongeza uzalishaji na hatimaye wawe na viwanda vidogo hata vya kukamua mchuzi wa zabibu,uzalishaji wa mkataba pia kuwa na viwanda vitakavyonunua moja kwa moja zabibu kutoka kwa wakulima.

Mtaalamu wa kilimo cha zabibu,Isaya Mng’ong’o alisema wakulima wamejifunza mwongozo wa kuzalisha zabibu kwa kanopi.

Alisema kuwa kanopi ni mfumo wa kuelekeza na kutandaza matawi ya mzabibu juu ya waya au miundombinu maalum ili mmea upate mwanga, hewa na nafasi nzuri ya kukua.

Alisema kuwa mfumo huo huongeza ubora na mavuno ya zabibu.na kupunguza magonjwa kutokana na mzunguko mzuri wa hewa

Pia hurahisisha uvunaji na kunyunyizia dawa, huongeza ubora wa matunda na sukari kwenye zabibu

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *