Na. Hafidhi Ally – Iringa
Wananchi wa Tarafa ya Pawaga Kata ya Itunundu Wilaya ya Iringa Vijijini wamejitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Isimani ambapo Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Emmanuela Mtatifikolo ameanza rasmi kunadi sera.
Akizungumza wakati wa kampeni hizo Bi. Mtatifikolo amesema kuwa atahakikisha wananchi wa jimbo hilo wanapata maendeleo kwa kuendeleza agenda zilizoanzishwa na mtangulizi wake Hayati Wiliam Lukuvi zikiwemo sikimu ya umwagiliaji, na ujenzi wa barabara ya Iringa mpaka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh. Jackson Kiswaga ambaye alishiriki kumnadi mgombea huyo amewataka wananchi kumpigia kura jwa wingi Bi Mtatifikolo kwani ni kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza na kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Kwa upande wao, wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Kampeni wengi wao wakiwa ni wana CCMÂ wameeleza kuwa na imani kwa Mgombea Ubunge huyo Bi. Emmanuela Mtatifikolo katika kuleta Maendeleo na kukuza uchumi wa Wananchi wa Jimbo hilo.
Iringa inafanya uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Ismani baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu William Lukuvi ambapo Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Juni 1, 2026.






