Rais Samia azindua ujenzi wa SGR kutoka Tabora hadi Kigoma

Na. Gerwin Kwigize, Kigoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendo kasi inayojengwa kutoka Dar es Saklaam hadi katika ukanda wa Magharibi na Ukanda wa Ziwa Victoria kwa lengo la kuinua uchumi wa taifa na kuunganisha Tnaznia na nchi nyingine za Maziwa makuu

Akihutubia Jana katika viwanja vya Katosho mjini Kigoma baada ya kuweka jiwe la Msingi,  Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameweka bayana kuwa hatua hiyo inalenga kuinua Uchumi wa kikanda kati yaTanzania na nchi za jirani kwa kuunganisha Ziwa Tanganyika na Bandari ya Dar es salaam

Hatua hii itafungua mlango mkubwa wa kibiashara baina ya mataifa hayo yenye utajiri mkubwa wa madini, huku ikitarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za usafirishaji wa mizigo kati ya bandari ya Dar es Salaam, Burundi na DRC.

Rais Samia anabainisha kuwa Reli hiyo inakusudiwa kuongeza fursa za ajira na kurahisisha utoaji wa huduma huku akitaja kuwa lengo ni kuunganisha usafirishaji majini na kwa njia ya reli akitangaza uzinduzi iwa Meli za mizigo katika bandari ya Kigoma

Wakazi wa Mkoa wa Kigoma na maeneo jirani wameshuhudia tukio la kihistoria la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameweka jiwe la msingi na kuzindua rasmi ujenzi wa mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kipande cha Tabora–Kigoma

Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 506 (kati yake kilomita 411 ni njia kuu na kilomita 95 ni matawi) itakapokamilika, itaunganisha Bandari ya Dar es Salaam na Ziwa Tanganyika, kisha kuendelea hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupitia njia ya Uvinza–Msongati–Kindu.

Also Read  Projects Launched to Reduce Conflicts Around reserved Areas

Pamoja na miradi hiyo Rais Samia ametoa tahadhari kuhusu masuala ya Usalam awa rai ana mali zao ili uwekezaji unaoendelea uwe na tija na endelevu

Uzinduzi wa Lot 6 unakuja ikiwa ni hatua nyingine ya kutimiza ndoto ya muda mrefu ya Tanzania ya kuwa na mtandao kamili wa reli ya kisasa yenye jumla ya kilomita 2,201 kote nchini, unaounganisha Dar es Salaam hadi maeneo ya Ziwa Victoria na mipakani mwa nchi jirani.

Tayari sehemu kadhaa za mradi huu mkubwa  ikiwemo Dar es Salaam–Morogoro, Morogoro–Makutupora, na Makutupora Tabora zimekamilika au zinaendelea kutekelezwa, huku Serikali ikiendelea kuwekeza zaidi ya dola bilioni 10 kwenye mradi mzima wa SGR kama sehemu ya mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa SGR kutoka Tabora hadi Kigoma ulitanguliwa na tukio la uzinduzi wa Meli nne za mizigo uliofanyika katika Bandari ya Kigoma, ambapo Rais Samia alipongeza wadau wa maendeleo na wawekezaji kutoka China ambao wamedhamiria kutumia bandari za Kigoma na Karema kwa ajili ya kusafirisha shehena za mizigo mbalimbali kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  ikiwemo madini kwenda bandari ya Dar es Salaam kupitia Ziwa Tanganyika na Reli ya Kati.

Awali akimkaribisha Mhe. Rais, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameeleza kuhusu mkakati wa wizara hiyo na namna utekelezaji unavyoendelea

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Sirro, ameeleza kuwa mradi huu utaboresha kwa kiasi kikubwa muunganiko wa kikanda na kufungua fursa nyingi za kiuchumi kwa wakazi wa Kigoma na maeneo ya Magharibi mwa nchi.

Also Read  TRA yatamba kwa miaka 30 ya mafanikio ya ujenzi wa Uchumi

Kazi za ujenzi tayari zimeanza na zimefikia zaidi ya asilimia 10, huku mkandarasi CCECC (China Civil Engineering Construction Corporation), akisimamiwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), akiendelea na kazi hizo.

Aidha Hatua za ujenzi wa Reli ya kuunganisha Tanzania ina Burundi uliozinduliwa mwaka 2025 katika eneo la Msongati mkoani Burunga nchini Burundi na Rais wa Burundi Mh. Everiste Ndayishimiye kwa pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Samia nao umeanza katika eneo la Uvinza na Kasulu nchini Tanzania.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *