Bulaya aahidi kutowaacha waandishi wa habari

Na. Mwandishi wetu

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya amekiri kuwa waandishi wa habari ni nyenzo mhimu ya maendeleo ya Taifa

Akizungumza katika kongamano la waandishi wa habari vijijini linalofanyika mjini Dodoma, Bulaya amesema anajivunia kuwa mwaandishi wa habari.

Amebainisha kuwa mafanikio aliyonayo yanatokana na misingi aliyoiishi katika tasnia ya habari ya udadisi, na kujali maslahi ya umma hasa vijijini

Ametoa wito kwa waandishi wa habari kujikita katika uandishi wa habari wenye kugusa maslahi ya Umma hasa wanaoishi na kufanya kazi za uchumi vijijini

Bulaya ameahidi kushirikiana na chama cha waandishi wa habari vijijini RUJAT na atatoa mchango wa hali na mali kwa Chama hicho ili kifanikishe malengo yake.

Kabla ya kuwa mwanasiasa na Mbunge kwa mihula minne, Bulaya alifanya kazi ya Uandishi wa habari katika vyombo mbalimbali ikiwemo Uhuru na Mzalendo.

About The Author

Also Read  Umeme Benaco kwenda Kyaka sasa rasmi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *